Thursday, 27 February 2014

HUMAN PAPILOMA VIRUS INFECTION.

Ugonjwa huu husababishwa na kirusi aitwaye HPV(Human Papiloma Virus), kuna aina 90 za kirusi huyu lakini aina 4 ndio huonekana mara kwa mara(HPV-6, HPV-11, HPV-16 na HPV-18) Mara nyingi husababisha viotezo mfano kwenye picha inaweza kua kimoja au vingi mfano hapo kwenye picha, hutokea sehemu za haja ndogo, kubwa na sehemu za uzazi(uke, uume, mfuko wa uzazi) Dalili huonekana kuanzia miezi 3 mpaka miaka 2 baada ya maambukizi...

Kuzaa

Vifo vya akina mama wakiwa na Mimba Vinapungua! Utafiti wa mwaka 2010 wa Hali ya Afya ya Jamii  (UHAJ)  waonyesha mafanikio huduma za Uzazi Utafiti wa Hali ya Afya ya Jamii 2010 (UHAJ) au kwa Kizungu DHS unaonyesha mafanikio makubwa hasa katika nyanja nne: mahudhurio  ya kliniki wakati wa kujifungua, kujifungulia hospitali, kujifungua ukisaidiwa na mhudumu wa afya yaani nesi au daktari na kupunguza vifo vya akina mama...

Maambukizi Yanayosambazwa kwa Kujamiana (MYKK)

Tunaelezea kwenye safu hii maambukizi yanayosambazwa kwa kujamiana. Wasomaji wengi wamezoea kuyaita magonjwa ya zinaa lakini habari hii inataka tubadilishe tuyaite ‘Maambukizi Yanayosambazwa kwa Kujamiana (MYKK)’ na tutaelezea kwa nini.  Wanaojua Kizungu labda watakumbuka kuwa hapo awali tulikuwa tunaita hali hizi ‘Sexually Transmitted Diseases (STD). Ukitafsiri moja kwa moja maana yake ni Magonjwa Yanayoambukizwa Kujamiana ....