Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Friday, 29 November 2013

MMMHHH HII KALI...!! MAITI HUFUKULIWA MAKABURINI ILI KUBADILISHWA NGUO KATIKA KISIWA CHA SULAWESI HUKO INDONESIA..

Image

Image 

KILA mwaka huko kaitika kisiwa cha Sulawesi, Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo na kuwatembeza kijini hapo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila ya ajabu inayoiitwa Ma’nene  ambayo wanaamini mtu akifa bado yuko nao kwa hiyo inawalizimu kufanya mambo hayo kama kuwabadilisha nguo.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”

Mpasuko Chadema sasa Baraza kuu

BAADA ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kufunga mjadala wa mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho, agizo hilo limeonekana kufuatwa vema na wajumbe wa Kamati Kuu, lakini limewafungua wajumbe wa Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na taasisi za chama hicho.
Tayari imeripotiwa kuwa uamuzi wa chama hicho kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo, umeipasua Kamati hiyo katika vipande vya wafuasi wa wagombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi ujao, Mwenyekiti wa sasa Taifa, Freeman Mbowe na Zitto.
slaa22
Miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu wanaotajwa kumwunga mkono Mbowe ni Dk Slaa, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu, Msemaji wa Chama hicho, John Mnyika na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Waliojitokeza waziwazi kumwunga mkono Zitto ni Dk Mkumbo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambao kwa hatua hiyo wamevuliwa nyadhifa zao na aliyekuwa Mwanasheria wa Mbowe, Albert Msando ambaye sasa ni Mwanasheria wa akina Zitto.
Wengine wanaotajwa kumwunga mkono Zitto ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti , Said Arfi ambaye uamuzi wa kumvua Zitto madaraka, ulisababisha ajiuzulu nafasi hiyo.
Hata hivyo, Profesa Mwesiga Baregu, ameripotiwa kukionya chama kwa hatua hiyo, akisisitiza kuwa baada ya uamuzi huo wa Kamati Kuu dhidi ya Zitto, chama kilitakiwa kisubiri baraka za Baraza Kuu, ndipo uamuzi huo utangazwe.
Wafuasi Baraza Kuu Jana Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, alitoa kauli iliyodhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa wanaomwunga mkono Zitto.
Joseph katika kauli yake, alionekana kuungana na Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Geita, Abdalah Hamis, ambaye hakumung’unya maneno, kwani aliweka wazi kuwa yeye atamwunga mkono Zitto. Mwenyekiti huyo wa Temeke, aliitisha mkutano na waandishi wa habari akimtaka Mbowe, kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza Kuu, ili litoe uamuzi sahihi kuhusu Zitto na wenzake.
Pamoja na kuwa yeye si mjumbe wa Sekretarieti ya chama, inayopanga ajenda za Baraza Kuu, Joseph alisema ajenda ya kikao cha Baraza hilo, ni kutaka viongozi wawaeleze wajumbe kwa nini wamesambaza waraka wanaodhani unawadhalilisha Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wakati waraka huo umekidhalilisha chama kwa kuonesha udhaifu wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu.
Akionekana kuwasemea wajumbe wenzake wa Baraza hilo, Joseph alisema katika mkutano huo, wajumbe watataka waelezwe kwa nini wasiamini kwamba uamuzi huo umeathiriwa na hofu ya uchaguzi wa ndani wa chama.
Pia watataka sababu zilizoifanya Sekretarieti ya Kamati Kuu, itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani, baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi, mpaka kuwavua uanachama.
Mjumbe huyo bila kuonesha hofu ya kuvuliwa madaraka kama wenzake walivyofanyiwa, alisema umefika wakati wa kuijenga Chadema bila kufuata masuala ya ubaguzi wa kidini, kikabila ama kikanda kama ambavyo inajulikana nje. Akifafanua hoja hiyo ya ubaguzi, alisema kuwapo kwa Zitto na Arfi katika nafasi za viongozi wa kitaifa, ilikuwa ni ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama.
“Sasa inawezaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia kuwa ni ishara kwamba hakuna udini?”
Alihoji Mwenyekiti huyo wa Chadema Temeke, na kusisitiza kuwa hayuko tayari kuburuzwa wala kuruhusu baadhi ya viongozi waendelee kuibomoa demokrasia wanayoitangaza kila kukicha.
Joseph alisema chama chao kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila kinapokaribia kwenye uchaguzi wa ndani hali inayosababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwa viongozi kwa kuitana wahaini na wasaliti.
Alisema amefadhaishwa na uamuzi wa Kamati Kuu dhidi ya Zitto na Dk Mkumbo, kwani haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufanya hivyo na kuutangaza kwa umma.
Kauli hiyo ya Joseph, ilitolewa pia na Dk Mkumbo, Msando ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu na Profesa Baregu. Hata hivyo, imekuwa ikipingwa na Lissu kwa kutumia Katiba hiyo hiyo ya Chadema, kwamba kuna kipengele kiliongezwa katika Katiba ya sasa, kinachoruhusu Kamati Kuu kuchukua uamuzi kama huo inapoona inafaa.
Joseph alisisitiza kuwa haingii akilini chama kinachopanga mikakati ya kushika Dola, kifukuze na kuogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.
“Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi operesheni zetu za chama ikiwemo ya M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nayo ni mikakati ya chama kushika Dola,” alisema Patrick. Mikoani Juzi Katibu wa Mkoa wa Geita, Hamis alitamka:
“Nikiwa Katibu wa Chadema, Mkoa wa Geita nasema mimi na wenzangu pia wote ndani ya mkoa wetu tutakuwa nyuma ya Zitto. Nyakati za uonevu, manung’uniko na kubaguliwa sababu tu za eneo, ukanda, udini na kuchaguliana marafiki zimekwisha.”
Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Tanga, Harid Rashid, ambaye alifuatana na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Hussein Baruti na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Tanga, Mohamed Aufi, aliripotiwa kusema hakubaliani na uamuzi wa Kamati Kuu.
Rashid alisema Kamati Kuu ilikuwa na njia nyingi za kulipatia ufumbuzi jambo hilo badala ya kuwavua uongozi. Alisema wameamua kuwa wazi kuhusu tukio hilo kutokana na ukweli kuwa Zitto ni mtu muhimu katika uongozi wa chama.
Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Zitto jijini Mbeya nao wanadaiwa kurushiana makonde na viongozi wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana misimamo kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu. Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mbeya Mjini, David Mwambigija ‘Mzee wa Upako’, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi mchana.
Mjadala wafungwa Kudhihirisha kuwa wajumbe wa Kamati Kuu wametii agizo la Dk Slaa la kufunga mjadala huo, jana gazeti hili lilipotafuta namna ya kumpata Mwigamba, alikuwa akikata simu zake.
Lilipomtafuta Profesa Baregu, alipokea lakini alijibu kwa ufupi kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia mambo ya Chadema. Wafuasi wa Mbowe Baada ya Zitto na Dk Mkumbo kuzungumza baada kuvuliwa madaraka, Mnyika na Lissu waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha yote yaliyozungumzwa.
Katika mkutano wao akina Mnyika, walidai kuwa waraka uliochapishwa na magazeti kuwa ndio uliomponza Zitto kwa kuwa si uliowasilishwa mbele ya Kamati Kuu.
Lakini mwandishi wa waraka huo, Mwigamba alijibu haraka kuwa hakuna kilichohaririwa bali waraka huo ndio sahihi. Kutokana na vurugu zilizotokea Kigoma, wafuasi wa Mbowe walisema ni za kutengeneza na leo wamejipanga kufanya mkutano kutetea hoja kuwa Kigoma anakotoka Zitto, wanaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu.
Mbali na kikao hicho cha Kigoma, pia Mratibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chasso), Dar es Salaam, Elihuruma Himida, alisema leo umoja huo utatoa kauli kupinga matamko ya wanaojiita wanafunzi wa vyuo vikuu, waliosema watazunguka nchi nzima kumwunga mkono Zitto.
Elihuruma pia alidai kuwa mkutano wa Zitto kujibu hoja za kuvuliwa madaraka, uliandaliwa na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), akina Juliana Shonza, waliohudhuria mkutano huo wa Zitto, huku viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), wakizuiwa kumsikiliza kiongozi huyo.
Source:Habarileo

Hivi Ndivyo DIANOND Alivyowafanyia Usaili Waliotuma maombi ya Kujiunga kundi lake la WCB-WASAFI..




Siku ya jana tulifanya zoezi la kuwafanyia interview
 baadhi ya watu waliotuma maombi yao kwa
 mujibu wa ,tangazo la kazi nilillolitoa
                                                                      juzi,mwitikio
 wa watu ulikuwa mkubwa,watu waliotuma
 email zao pamoja simu,kiasi ilituwia vigumu 
kuwataka wote waje kwenye interview,ilitubidi
 tuchague baadhi ya watu ambao tulihisi wanaweza
 kukidhi sifa tulizozihitaji ingawa nao pia tulipata
 changamoto ya wengi wao kuja pasipo kuzingatia maelekezo 
 na maagizo ya tangazo lilivyotaka,hivyo jana 
nikishilikiana na wataalamu wa hizo sekta tulisaili
 na mwisho wa siku tutachukua wale wenye viwango
 tunavyovihitaji na kuungana na team ya WCB-WASAFI,.....
Ahsanteni sana

WATANZANIA WAWILI WANASWA NA SHEHENA YA KILO 55 ZA MADAWA YA KULEVYA HUKO AFRIKA KUSINI...!!



Johannesburg/Dar. 
 Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya. 


Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).

Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.

Msemaji wa Hawks, Paul Ramaloko alisema jana kuwa maofisa hao walivamia nyumba waliyokuwa wanaishi Watanzania hao na kukuta mzigo huo.

Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watu hao kwa kuhofia kuharibu uchunguzi akisema bado walikuwa wanawasaka watuhumiwa zaidi wakiwamo raia wa Afrika Kusini.

Alisema kikosi chao kimepata mafanikio makubwa kwa kukamata dawa nyingi kiasi hicho... “Tunakaribia kuwakamata vinara wa biashara hiyo, maana tumeelezwa kuna kundi kubwa la watu wazito,” alisema Ramaloko. Hii inakuwa mara ya pili katika kipindi cha miezi minne kwa Watanzania kutuhumiwa kubeba dawa hizo.

Julai mwaka huu, wasanii wawili Agness Gerald `Masogange’ na Melissa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Johannesburg wakiwa na kilo 180 za kemikali aina ya ephedrine zenye thamani ya Sh7 bilioni.

Baada ya kukaa miezi miwili jela, Masogange alipatikana na hatia ya kuingiza kemikali hiyo, ambayo hutumika kutengeneza dawa za kulevya na kutozwa faini ya Rand 15,000 (Sh2.3 milioni).

Melissa aliachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia.

Wasafirishaji sasa watumia samaki

Katika hatua nyingine, wasafirishaji wa dawa za kulevya inasemekana wamebuni mbinu mpya ya kutumia samaki kusafirisha bidhaa hiyo haramu.

Akizungumza jana wakati wa uteketezaji wa dawa za kulevya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema wanatumia samaki kwa kuwa wana harufu kali.

----Mwananchi

KAPUYA HAKAMATIKI....ATUA JIJINI DAR KWA MBWEMBWE, POLISI WAMGWAYA..

HATIMA ya Mbunge wa Urambo Magharibi Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, amerejea nchini jana akitokea nchini Sweden, huku Jeshi la Polisi likikwama kumtia mbaroni kama lilivyokuwa likitamba.  
 
Wakati mbunge huyo akiwasili nchini na kupokewa na kusindikizwa na wapambe wake, Bunge limeridhia kukamatwa kwake kwani tuhuma zinazomkabili ni za jinai na zinamhusu yeye binafsi.
  
Mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, amerejea nchini jana majira ya saa tano asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar na kutua katika uwanja huo wa ndege na kuondoka kupitia mlango wa watu maarufu (VIP).
 
Habari zinasema mbunge huyo alipoondoka katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere alikwenda moja kwa moja kwenye moja ya hoteli za jijini Dar es Salaam na kuacha mizigo yake, kisha kuondoka na gari namba T 104 AEZ Toyota, huku wapambe wake wakiwa katika gari namba T 170 BGY aina ya Benz.
 
Wakati Kapuya akitua katika uwanja huo wa ndege, polisi ambao kwa takriban wiki moja sasa wamekuwa wakitamba kutaka kumtia mbaroni mara baada ya kutua, baadhi yao walionekana wakisalimiana naye kama vile hawakuwa wanamuwinda.
 
Tangu Profesa Kapuya alipoondoka nchini huku akizongwa na kashfa ya kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, polisi wamekuwa wakitamba kutaka kumtia mbaroni na kuahidi kuwa mara baada ya kurejea nchini mbunge huyo angekuwa chini ya ulinzi.
 
Tanzania Daima juzi liliripoti mkakati wa polisi kutaka kumtia mbaroni mbunge huyo mara atakapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilisema kuwa kumekuwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya jeshi hilo kutaka waziri huyo wa zamani ahojiwe kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka.
 
Hatua ya polisi kutaka kumnasa Kapuya akiwa uwanja wa ndege inadaiwa kuchangiwa na taarifa ya  wiki iliyopita kwamba baadhi ya vigogo wa jeshi hilo walishiriki kufanikisha safari ya mbunge huyo nje ya nchi huku wakijua fika anatakiwa na polisi.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa kuhusu ujio wa Kapuya na kisha kuendelea kuachiwa huru, alisema yuko nje ya Jiji la Dar es Salaam na hakuwa na taarifa za kurejea kwake.
 
Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Yusuph Mrefu, alipoulizwa kuhusu sakata la Kapuya, alisema hakuwa na taarifa ya kile kinachoendelea, kwa kuwa ndiyo kwanza amekabidhiwa ofisi.
 
“Mimi niambie jambo jipya, hapa ofisini ndiyo leo nimeingia kukaimu, sasa hayo mambo nitayajulia wapi, ni vema ungeniambia jambo jipya tuweze kutatua,” alisema Mrefu.
 
Kwa upande wake, Bunge limesema kuwa sakata la Profesa Kapuya lilifikishwa bungeni na kubaini kuwa ni la jinai, hivyo linapaswa kwenda kwenye mkondo wa kisheria.
 
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, alithibitisha kulifahamu suala hili, kwani binti aliyedai kubakwa na kutishiwa kuuawa na mbunge huyo alikwenda bungeni wakati Bunge la 13 lilipokuwa likiendelea mjini Dodoma.
 
“Suala la binti huyo lilifikishwa ofisini kwangu kupitia kwa msaidizi wangu ambaye  alisikiliza hoja na rai yake na kushauriwa kuwa hilo ni suala la jinai na linapaswa liende katika mkondo wa kisheria, hata hivyo binti huyo alitambulishwa kwa Spika kama kiongozi wa wabunge na kuelekeza kuwa tumshauri alifikishe katika mamlaka husika,” alisema Kashilila.
 
Tayari binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa ameshafungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam na Jeshi la Polisi likaahidi kumkamata Kapuya popote alipo ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
 
Tayari makachero wa polisi wameanza kufuatilia namba ya simu inayodaiwa kutumika kumtisha binti huyo na wakati mwingine kutumika kurusha pesa kwa njia ya mtandao, zinazodaiwa kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo.

Credit-Tanzania Daima

HII NDIO GARI AINA YA RANGE ROVER VOGUE AMBAYO NI NDEFU KULIKO GARI ZOTE AFRIKA MASHARIKI...ITAZAME HAPA..

5921_643916678955211_694058705_n-4570-600-600-80 

Mara nyingi tumezoea kuziona Limousine ndefu kwenye wedding tofauti lakini Range hii ambayo ipo Kenya inaweza kuwa ndio ndefu zaidi kuliko Range zote ambazo zipo Africa Mashariki. Watu wangu mnaopenda magari enjoy kuangalia hizi picha saba za hili gari.


58873_618020604878152_762034716_n-4569-600-600-80 64755_590187184328161_235651424_n-4568-600-600-80 226879_590182380995308_543629288_n-4565-600-600-80 (1) 
383670_557935277553352_1184415968_n-4571-600-600-80 529115_615751478438398_1881184687_n-4566-600-600-80 545705_590182444328635_1651343247_n-4564-600-600-80




Tuesday, 26 November 2013

Watoto watekwa , walawitiwa na kuteswa kinyama ndani ya handaki lilipo katika msitu wa Mabwepande..

 

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.

Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.

Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.

Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.

Walisem a   w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.

"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.

"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.

Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.

"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.

"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel

Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.

"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.

"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.

"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.

"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.

Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.

Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.

Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.

"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.

Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.


-Gazeti la Majira.



TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI JANA KATIKA MKESHA WAKUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA.

likua ni mwezi november tarehe 26 mwaka 2012 majira ya sa 2 usiku ndipo ziliposambaa taarifa za kifo cha muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ Husein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’.
Leo tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya kumkumbuku ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga.
DSC01943wanafunzi wa madrasa wakiimba kaswida kwenye mkesha huu wa kumuombea marehemu Sharo Milionea
Jana tarehe 25 november kulikua na mkesha maalum,Mkesha huu umeambatana na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa madrasa,Miongoni mwa watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
DSC01971Mama mzazi wa sharo milionea katikati ya kitale na rafiki wa kitale
millardayo.com imepiga exclusive interview na mama mzazi wa Sharo Milionea pamoja Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel,Azam pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
DSC01901
‘Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka sasa mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa jumla ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na mjomba wake,nikamwambia mjomba wake akiuze  kwa sababu ya usumbufu maana mi nipo mbali huku,maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
gariii
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa marehemu kwa hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli Mudy Suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa hiyo movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa ni movie moja ambayo amecheza yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo
DSC01892
DSC01943
DSC01939

Friday, 15 November 2013

INASHANGAZA....!! KABURI LA BABA’KE BAHATI BUKUKU LAZIKIWA MGOMBA..


Ni fedheha sana msibani!

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku hivi karibuni alipatwa na simanzi kubwa baada ya aliyekuwa baba yake mdogo, Lwaga Bukuku kufariki dunia, lakini wakati kaburi likiwa limechimbwa Sinza Makaburini, iliamriwa msiba huo usafirishwe kwao Mbeya na hivyo kusababisha shimo hilo kuzikwa mgomba badala ya mwili wa mtu.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 7, mwaka huu, huko Tabata Kisukuru wakati waombolezaji waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanatoa heshima za mwisho kwa marehemu ambaye alikuwa akazikwe kwenye Makaburi ya Sinza, jijini Dar es Salaam ambako tayari kaburi lake lilishachimbwa.

Lwaga, baba mdogo wa mwimbaji huyo ambaye muda wote wa kuumwa kwake alikuwa akiuguzwa naye, alifikwa na umauti Novemba 5, mwaka huu akiwa Hospitali ya Kadinary inayomilikiwa na Dk. Mvungi iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam na baada ya kifo chake, shughuli za msiba zilihamia nyumbani kwa Bahati Tabata Kisukuru.

-GPL


HII NDIYO TV INAYOUZWA MILIONI 75 ZA KIBONGO, IPO MLIMANI CITY...IFAHAMU ZAIDI KWANINI INAUZWA BEI KUBWA ..

Niliwahi kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata watatumia kwenye nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na kununua gari huku wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.
Sasa basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa kufanya mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha pesa kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya inch 85 na usirudishiwe chenchi.
tovuti hii ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii ina vitu vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na sura kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya kutumia remote. 104 
Smart contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyingine
 mbalimbali ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati mmoja.
Ina music system yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna haja ya kununua home theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila decorder na ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo unaiweka kwenye smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
105
102
101

Monday, 11 November 2013

'PANYA MWOKOZI WA MAISHA, soma hapa upate kufahamu!!!


'Panya mwokozi wa maisha'

Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.

Uwezo kutokana na maumbile ya pua

Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko.Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine,Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji. Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.

Kutafuta hatua kwa hatua

Panya hujifunza kufuta eneo fulani hatua kwa hatua. Waya au kamba hufungwa mwilini kutoka kwenye ufito. Wasimamizi wawili husimama kila upande wa ufito na kumruhusu panya kutembea toka mwanzo wa ufito hadi upande mwingine kwa kufuata jinsi waya au kamba alizo fungwa mwilini. Katika mafunzo ya awali panya hufunzwa kunusa kemikali aina ya TNT ndani ya chombo cha chuma.

Kugundua mabomu ardhini

Baadaye kila panya hufanya mafunzo kwenye eneo ambalo kuna mabomu ya ardhini yaliyofukiwa na vifaa ambayo huzuia mlipuko. Ikiwa panya ameweza kunusa na kutambua yalipo madini asilia ya TNT huwa anasimama na kuanza kufukua sehemu hiyo ya ardhi iliyofukiwa bomu. Kuwafundisha panya kunachukua muda wa mwaka na inagharimu dola za Kimarekani $6,000 sawa na Euro 4,670.

Zawadi kwa ufanisi

Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi. Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu.

Pua za kunyumbulika

Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa. Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote. Hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola,Thailand na Kambodia.

Sunday, 10 November 2013

Je! unamjua FARAO/ FIRAUNI wa enzi za MUSA? Mwili wake wapatikana, tazama hapa umwone!!!!!

FIRAUN LANATULLAH

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Saturday, 9 November 2013

AL SHABAAB WARUDI TENA!!!: 'WAKIRI KUHUSIKA KULIPUA HOTELI....WATU 6 WARIPOTIWA KUPOTEZA MAISHA....SOMA ZAIDI




Wapiganaji wa Kiislam wa Al Shabaab nchini Somalia

Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somali wamesema wao ndio waliotekeleza shambulizi la bomu la kujitoa muhanga nje ya hoteli katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia ambapo watu sita waliuawa wakiwemo maafisa wa polisi.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amelaani shambulio hilo lilitokea nje ya Hotel ya Maka al Mukurama huku akisisitiza kuwa shambulio halitarudisha nyuma jihada kubwa zinazoendelea za kuleta amani na usalama nchini humo.

Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya mashambulizi.

Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.

Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.

Friday, 8 November 2013

HII NDIO AJALI YA PIKIPIKI ILIVYOCHUKUA ROHO ZA WANACHUO WAWILI WA CBE DODOMA

WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara   wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo  yenye namba za usajili T 420 CCN  waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE  na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo  na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa

lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia
 Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
 Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani hapo.
 
 Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Dodoma.
 Askari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.

Wednesday, 6 November 2013

BREAKING NEWS...!! DJ RANKEEM AFARIKI DUNIA LEO MCHANA.

 

Dj Rankeem Ramadhan enzi za uhai wake.

  Dj Rankeem Ramadhan amefariki dunia leo mchana. 

Marehemu aliwahi kufanya kazi Radio One, Clouds FM, Radio Free na kupiga disco katika kumbi mbalimbali. 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

Monday, 4 November 2013

ANGALIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA (SOLAR ECLIPSE) LILIVYOTOKEA HAPO JANA KUTOKA NCHI MBALI MBALI..!!



Siku ya jana Jumapili jua ilikuwa ni siku ya kupatwa kwa jua ( solar eclipse)na hivi ndivyo ilivyoonekana katika sehemu mbalimbali za Dunia Picha hapo juu ilivyoonekana huko Somalia na chini ilivyokuwa nchini Kenya.

 

Saturday, 2 November 2013

MAMBO MAKUU MATANO USIYOFAHAMU KUHUSU MTANDAO WA FACEBOOK...SOMA HAPA NIKUJUZE...



Mtandao wa kijamii wa FaceBook ni miongoni mwa mitandao yenye wafuasi wengi na unaopendwa zaidi Dunia, Kwa historia fupi ni kwamba mmuanzilishi wa Facebook ni kijana mdogo anayefahamika kwa jina la Mark ZuckerBerg(29) ambaye asili yake ni Raia wa Israel anayeishi nchini marekani.
Haya ni mambo makubwa matano usiyoyafahamu kuhusu mtandao wa Facebook.
(1.) Idadi  ya watumiaji wa mtandao wa Facebook Dunia(Active Users) ni Milioni 901 kwa mwaka huu ukilinganisha na miaka michache ya nyuma ambapo idadi ilikuwa ni watumiaji Milioni 680.
(2.)Kila siku jumla ya   Picha Milioni 300 huwa zinakuwa zinapakiwa(UPLOADED) katika mtandao wa Facebook.
(3.)Jumla ya LIKES na COMMENTS Bilioni 3.2 zinazokuwa posted katika mtandao wa Facebook kwa siku.
(4.) Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba MAPATO yatokanayo na mtandao wa Facebook kwa robo ya mwaka jana wa 2012 ni jumla ya Dola Bilioni 1.058, kutoka Dola Milioni 730 ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita.
(5.) Kwa sasa mtandao wa Facebook unawafanyakazi wapatao 3,539 ambao wapo katika ajira ya kudumu(Full-Time Employees).