Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Friday, 29 November 2013

HUKUMU YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 18 KARIBU NA IKULU DAR ES SALAAM...SOMA ZAIDI..

HUKUMU ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji wa kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu Dar es Salaam, inayowakabili vigogo wawili wa Wakala wa Ujenzi itatolewa Januari 15 mwakani.


Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Sundi Fimbo alisema hayo jana baada ya washitakiwa kumaliza kujitetea.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wamejitetea bila kuita mashahidi ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga.


 

Ikulu inavyoonekana ukiwa juu ya jengo.

Awali akijitetea Maliyaga alidai kuwa, Mkurugenzi wa Miliki wa Wakala, Charles Makungu ndiye aliyekuwa na uamuzi wa mwisho wa kutoa kibali cha ujenzi na kupeleka barua katika halmashauri husika na kwa waleta maombi.

Akiongozwa na Wakili Majura Magafu, Maliyaga alidai alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kutoa Vibali na walipopata ombi la ujenzi huo walipitia michoro na baada ya kuona ipo sawa alisaini kibali na kupeleka kwa Makungu.


Alidai kuwa awali aliandika barua akipendekeza ofisi ya Makungu iombe kibali kutoka Halmashauri ya Ilala lakini hakupata majibu hadi alipopewa maelekezo kutoka katika kamati inayoshughulikia miradi ubia kuwa watoe kibali hicho. Alidai alikataa kutoa kibali hicho lakini baada ya wanakamati kujadili walikubali kufuata maelekezo hayo na kutoa kibali hicho.


"Sisi hatukuhusika katika kutoa uamuzi wa mradi huu, mimi nimeonewa kwasababu sijanufaika na sikutumia madaraka yangu vibaya na nashangaa kwanini Makungu, watu kutoka katika kamati yetu au ile ya miradi ya ubia hawajaletwa mahakamani," alidai Maliyaga.


Katika utetezi wake hivi karibuni Kimweri alidai kuwa amefunguliwa kesi hiyo kwa kuwa alikuwa na ugomvi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli baada ya kumchafua kwenye vyombo vya habari.


Alidai ugomvi huo ulitokana na mchakato wa uuzwaji wa nyumba za Serikali ambapo yeye alikataa kusaini mkataba wa kumuuzia nyumba mwanafunzi kwa sababu hakustahili ndipo Magufuli alipodhani kuwa alitoa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.


Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.


Aidha wanadaiwa kutoa kibali kingine cha kuongeza ujenzi kutoka ghorofa 15 hadi 18.

-habarileo

Saturday, 16 November 2013

Umeme kuadimika kwa siku 11 nchini.... Na hii ndo mikoa itakayokumbwa na tatizo hilo...!!


WATEJA katika mikoa inayopata umeme kwenye gridi ya Taifa wanatarajiwa kupata adha ya upungufu wa umeme kwa siku 11 kuanzia leo, kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.
 
Hali hiyo imetajwa inatokana na kuwapo kwa matengenezo ya kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited (PAT).
 
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud aliyasema hayo Dar es Salaam jana, akisema upungufu huo utatokea kati ya Novemba 16 hadi Novemba 26, mwaka huu na itahusisha maeneo yaliyopo katika mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifa.
 
“Tumepata barua kutoka kwa kampuni ya Pan African inayotuuzia gesi, wakisema inafanya matengenezo hayo kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Masoud, kutokana na matengenezo hayo mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo na kwa nyakati tofauti na kuongeza huduma ya umeme ni muhimu kwa kila Mtanzania kwa ajili ya kujiinua kiuchumi na kipato, lakini matengenezo hayo ni muhimu kwani itaboresha upatikanaji wa gesi kwa ufanisi zaidi.
 
Aliitaja mikoa na maeneo yatakayokumbwa na upungufu wa umeme kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar.
 
Masoud alisema gesi imekuwa ikiwawezesha kutoa Megawati 100 katika kituo cha Ubungo 1, Megawati 100 katika kituo cha Ubungo 2, kituo cha Tegeta Megawati 45 wakati Kampuni ya Songas imekuwa ikitoa Megawati 182 na kuongeza kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa Megawati kati ya 150 na 200 na kwamba uzalishaji wa umeme kutumia mafuta na maji utaendelea.
 
Alisisitiza kuwa upungufu huo wa umeme sio mgawo ila ni kupitisha matengenezo ya kiufundi ya Kampuni ya Pan African ambayo alidai kuwa ilishaiomba Tanesco miezi miwili iliyopita ikitaka kufanya matengenezo hayo ambayo hayaepukiki na yenye lengo la kuleta ufanisi zaidi.
 
Masoud alitoa wito kwa wananchi kuwa wavumilivu siku hizo 11 wakati matengenezo yakifanyika na kuwa lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosha na kutoa huduma inayoridhisha ya nishati ya umeme kwa wateja wake.

-Habari Leo


MENO YA TEMBO YAWAPELEKA JELA MIAKA 70

MENO YA TEMBO YAWAPELEKA JELA MIAKA 70
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, katika Mkoa wa Katavi, imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka 70 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya Sh45 milioni.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na ule wa upande wa utetezi.
Waliohukumiwa kifungo hicho ni, Gwabi Mayala(39 mkazi wa Kijiji cha Majimoto katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
tembo
Mayala alikuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo na amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa fidia ya Sh. 45 milioni/=. Wengine waliohukumiwa ni Mashaka Mabanga (33) mkazi wa Sumbawanga katika Mkoa wa Rukwa na Adamu Kalinzi (30) mkazi wa Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele ambao kila mmoja amehukumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Mapema, Mwanasheria wa Serikali katika Mkoa wa Katavi, Fadhili Mwandoloma, alidai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo usiku wa Oktoba 10 mwaka huu katika Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele

MFAHAMU MSAIDIZI WA RAISI OBAMA ALIYEKULIA KOROGWE, Dodoma

VivekKundraPDC
WAKATI anaingia madarakani rasmi Januari 20, mwaka 2009 kuiongoza Marekani, nchi kubwa yenye nguvu za kiuchumi na kisiasa duniani, Barack Obama alikuwa na malengo mengi. Mojawapo ni kuzidi kuipaisha Marekani na kuwasuta waliodhani nchi hiyo haiwezi kuongozwa na mtu mweusi.
Itakumbukwa kwamba, Obama mwenye asili ya Kenya ambaye kwa sasa ni Rais wa 44 wa Marekani, ndiye mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwahi kuiongoza Marekani.
Hivyo, katika kuhakikisha anatimiza ndoto zake, alipanga safu imara ya wasaidizi, miongoni mwao aliibuka kijana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 35 tu, lakini aliyekuwa na kichwa adimu katika utundu wa kazi, hasa kwa upande wa teknolojia.
Huyu si mwingine bali ni Vivek Kundra aliyezaliwa huko New Delhi, India. Huyu alipewa jukumu la kuwa Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Serikali ya Marekani. Kundra, ingawa ana asili ya India, ni ‘Mswahili’ anayeijua vyema Tanzania, kwani amekulia Tanzania.
Historia yake inaonesha kuwa, akiwa na umri wa mwaka mmoja tu, yeye na wazazi wake, walihamia Afrika, katika nchi ya Tanzania. Baba yake alikuwa miongoni mwa maprofesa na walimu waliokuja nchini kufundisha katika shule kadhaa.
Kutokana na mpango huo, Kundra alijikuta akiishi na wazazi wake huko Korogwe, Tanga na pia mkoani Dodoma. Ni huko ndiko alikozama katika Kiswahili, akiifanya lugha yake ya kwanza huku Kihindi na Kiingereza zikiwa lugha za ziada kwake.
Aliishi Tanzania hadi alipofikisha umri wa miaka 11 ambapo wazazi wake walihamia Washington D.C, Marekani.
“Kwa hiyo ninaijua vizuri Tanzania na ninakifahamu vizuri Kiswahili,” anasema Kundra ambaye akiwa Marekani, alihitimu Shahada ya Kwanza katika Saikolojia aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Maryland Park.
Hakuishia hapo, alirudi tena darasani kusoma Teknolojia ya Habari katika Chuo Kikuu cha Maryland, lakini pia alisoma katika Taasisi ya Uongozi wa Siasa ya Sorensin ya Chuo Kikuu cha Virginia.
Kutokana na umahiri wake kitaaluma, Machi mwaka 2011 alitangazwa kuwa mmoja wa waliothibitisha vipaji vya uongozi duniani, akichaguliwa na jopo la wajuzi na wasomi kutoka Mkutano wa Uchumi Duniani (WEF).
Mwaka huo, katika mkutano uliofanyika Amman, Jordan, Kundra alikuwa mwenye furaha kukutana na kijana mwingine aliyepewa heshima kama yake, Susan Mashibe wa Tanzania ‘milionea mtoto’ ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya TanJet, kampuni ya kimataifa na ya kwanza ya aina yake nchini inayoshughulikia masuala ya kiufundi katika ndege binafsi, za biashara na hata za kidiplomasia.
Mwanadada huyu, pia anamiliki kampuni nyingine inayojulikana kama Kilimanjaro Aviation Logistic Center, ambayo inashughulikia taratibu za utuaji na urukaji wa ndege binafsi katika Bara la Afrika.
Aidha, ameanzisha Huduma ya Matengenezo na Ukarabati wa Ndege Kilimanjaro, kwa lengo la kutoa huduma za kisasa, yenye kiwango na salama katika usafiri wa anga wa jumla na ushirika katika eneo la Afrika. Lakini pia Susan ndiye Mwanamke wa Kwanza Afrika Mashariki mwenye Cheti cha Rubani cha FAA na Mhandisi Matengenezo wa Ndege.
Tangu kuanzishwa TanJet mwaka 2003, Mashibe ametunukiwa Tuzo mbalimbali ikiwemo ya Askofu Desmond Tutu ya mwaka 2009 na ile ya Mwanamke Mjasiriamali mwenye Mafanikio ya mwaka 2009.
Tukirudi kwa Kundra, mwaka mmoja kabla ya tuzo ya WEF, alituzwa na taasisi ya teknolojia ya SANS kwa kuwezesha kufichua wizi wa dola za Marekani milioni 300 (Sh bilioni 450) uliokuwa unafanywa kwa njia ya mtandao kwa takribani kila mwaka na baadhi ya watendaji serikalini.
Aidha, Kundra amewahi kutunukiwa Tuzo kemkem kutokana na umahiri wake katika miundombinu ya teknolojia na habari na mawasiliano, akiwa amegundua mifumo kadhaa ya kisasa. Ndiyo maana Chuo Kikuu cha Harvard hakikutaka kuuachia ujuzi wake, na hivyo kuamua kuingia naye mkataba wa kufundisha kwa mkataba chuoni hapo.
Nje ya kazi hiyo, Kundra pia ni Makamu Mwenyekiti wa kampuni kubwa ya masomo ya Salesforce ya Marekani. Majukumu mengine ya kitaaluma aliyokuwa nayo kabla ya kuitwa Ikulu ya Marekani kumsaidia Rais Obama ni kuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Teknolojia huko Arlington, Virginia mwaka 2001 na miaka mitano baadaye, aliteuliwa na Gavana wa Virginia, Tim Kaine kuwa mkuu wa shughuli za kiteknolojia jimboni humo.
Ilipofika Machi 27, 2007, Meya wa Columbia, Adrian Fenty alimteua Kundra kuwa Ofisa Teknolojia Mkuu wa Columbia.
Je, anazungumziaje kuaminiwa kwake na Rais Obama? Anasema: “Ni heshima kubwa. Sikuwaza kuwa msaidizi wa Rais katika nchi muhimu kama Marekani. Kama unavyojua, nilizaliwa India, nikakulia Tanzania.
Ni mhamiaji tu hapa na ikumbukwe nilikuja Marekani mwaka 1985 nikiwa sijui hata Kiingereza, zaidi ya Kihindi na Kiswahili.
“Lakini bidii katika masomo na nyanja ya utawala, vitu nilivyorithi kutoka kwa wazazi wangu, ndivyo vilivyonifikisha hapa, kiasi cha kuaminika na jamii na hata Rais wa nchi.Namshukuru Mungu kwa kila jema linalotendeka juu yangu. Namshukuru Rais Obama kwa kuwapa nafasi vijana pia.”
Huyo ndiye Vivek Kundra, mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano aliyekulia Tanzania, lakini sasa akifanya vitu vikubwa nchini Marekani.
Source: HabariLeo

Friday, 15 November 2013

YAGUNDULIKA..!! MTIHANI WA KIDATO CHA NNE- 2013 WAVUJISHWA..!! HII NI AIBU KWA TAIFA..


MTIHANI wa Taifa wa Kidato cha Nne, umeingia dosari baada ya walimu wawili akiwamo Mkuu wa Shule, kushikwa wakishiriki kutoa majibu kwa wanafunzi wao.



Tayari Polisi mkoani Singida, inashikilia walimu hao wa Sekondari ya Nkinto wilayani Mkalama kwa tuhuma ya kuvujisha mtihani huo unaoendelea kufanyika nchini kote hivi sasa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu wa Shule, Monica Sebastian (30) na msimamizi wa mtihani huo, Agaloslo Otieno (32).
Alisema watuhumiwa hao walivujisha mtihani huo juzi kati ya saa 3 na 3:30 asubuhi katika shule hiyo iliyopo Kata ya Mwangeza Tarafa ya Kirumi.
Alidai kuwa Mwalimu Agaloslo aliyekuwa akisimamia mtihani katika shule nyingine ya Mwangeza, aliandika baadhi ya maswali ya Kiswahili na Uraia kwenye simu yake ya mkononi na kumtumia Mkuu wa Shule yake ya Nkinto, Monica aliyekuwa shuleni kwake.
Baada ya Monica kupata maswali hayo, inadaiwa alitafuta majibu akiwa chooni huku wanafunzi wakimfuata huko huko na kupewa majibu.
Kamanda Kamwela alisema lengo lao lilikuwa kusaidia wanafunzi, wafanye vizuri katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu. Alisema wanafunzi waliishaambiwa wadanganye wanakwenda chooni, ili wakapewe majibu na Mkuu wa Shule.
"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa uvujishaji huo ulifanyika kwa nyakati tofauti kati ya Monica na Mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani huo katika shule tofauti.
“Baada ya Mkuu wa Shule kutumiwa maswali, alijificha chooni na watahiniwa kwa nyakati tofauti waliomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda kujisaidia na hapo walimkuta Mkuu wa Shule na kuwapa maelekezo ya namna ya kujibu maswali hayo," alisema Kamanda Kamwela.
Alisema baada ya Polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria, iliweka mtego katika Sekondari ya Nkinto na kumkamata Mwalimu Monica huku simu yake ikiwa na baadhi ya maswali ya mtihani.

-Habari Leo

HAYA NDIYO MATESO YA MAREHEMU DK. MVUNGI....

HADI anakata roho Novemba 12, mwaka huu, Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi amepitia mateso makubwa.

 

Dk. Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Novemba 3, mwaka huu alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani nyumbani kwake Kibamba-Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi).

Tangu lilipotokea tukio hilo, Dk.Mvungi aliishi katika mateso makubwa kutokana na kupoteza fahamu huku akipumua kwa kutumia mipira ya gesi hadi kifo kilipomfika katika Hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini.

 

Dk. Mvungi enzi za uhai wake.
Kwa takribani siku tisa, Dk. Mvungi alikuwa akisikilizia maumivu makali ya majeraha makubwa ya mapanga hivyo ni dhahiri kuwa alipitia mateso makubwa.

Watu kumi akiwemo John Mayunga ambaye ni mtuhumiwa wanaodaiwa kuvamia nyumbani kwa Dk. Mvungi wanashikiliwa na jeshi la polisi jijini Dar kwa ajili ya mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.
Watu hao walikamatwa wakiwa na mapanga pamoja na simu ya marehemu.

"KAPUYA HANA KOSA LA KUJIBU...HAYO NI MAMBO YAKE BINAFSI"...KAMANDA KOVA

 Akiongea na wanahabari leo mchana kamanda kova kasema hawawezi kumuita Mhe. Kapuya kasababu haya ni mambo yake binafsi na hakuna mtu yeyote ambaye amakuja hapa polisi kulalamika kutendewa vibaya na Mhe. Kapuya.
"hata hivyo kamanda kova kasema kama kuna ushahidi wowote wa kueleweka sio kusingizia mtu vituo vya polisi viko wazi masaa 24"


Kufuatia kashfa ya kubaka mwanafunzi wa sekondari: TAMWA, TGNP, LRHC wamtaka Professor Juma Kapuya wa CCM ajiuzulu ...!!


Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LHRC), kimelaani viongozi wanaotumia madaraka yao, nafasi zao na nguvu zao kisiasa kuwadhalilisha watoto wa kike.

Mashirika hayo yanayotetea haki za wanawake na watoto, yamesema yamesikitishwa na habari zilizozoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu wasichana wawili wanaotafuta haki yao dhidi ya kiongozi wa kiserikali anayetuhumiwa kuwadhalilisha. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka

 "Mashirika hayo yanafahamu kuwa vitisho vilivyotolewa na kiongozi huyo vimewasababishia wasichana hao kuogopa kuishi nyumbani kwao kwa kuhofia maisha yao," ilisema sehamu ya taarifa ya pamoja ya mashirika hayo.


Iliongeza: “Tunashangazwa kuona hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika wakati wasichana hao wakitafuta msaada," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,  Valerie Msoka, katika taarifa hiyo.


Masharika hayo yametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwalinda wasichana hao dhidi ya mtuhumiwa.
 
Aidha, ili kujenga imani na utawala bora, mashirika hayo yamemtaka mbunge huyo kujiuzulu mara moja.

Alisema Tamwa, TGNP na LHRC, yanawataka Watanzania kuungana na kupinga viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya. Watanzania wapige vita vitendo visivyo vya haki kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

CHANZO: NIPASHE.

Tuesday, 12 November 2013

INAHUZUNISHA ...!! DR. SENGONDO MVUNGI AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA MILPARK HUKO SOUTH AFRICA...SOMA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI..

Sengondo Mvungi 1 


Habari za kusikitisha zilizotufikia jioni hii zinasema kuwa Dk. Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7 kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Muhimbili kitengo cha Moi ambako muda wote alikuwa hajitambui baada ya kushambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya sehemu ya kichwani akiwa nyumbani kwake Kibamba

Ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi uliofanywa dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuz. 



Inauma sana!!! Taifa letu tuzidi kuliombea sana na tusikate tamaa!!!

Mungu ampokee na amweke pema!!!...R.I.P 

TUTAZIDI KUKUPA YANAYOJILI ZAIDI BAADAE ENDELEA KUWA NASI MDAU WETU..

Saturday, 9 November 2013

Rais Kikwete ampa RUNGU Waziri Magufuli...Amtaka aongezi ukali katika kusimamia sheria za Matumizi ya barabara zetu

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyeshika mkasi) akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John P. Magufuli na kulia kwa Rais ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Eng. Mussa Iyombe. Wengine katika picha ni baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa Mikoa ya Geita na Kagera walioshiriki katika sherehe hizo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Lori aina ya Scania la Kampuni ya MAP CO Ltd. likiwa na usajili namba T 895 AFH/T 226 AGB kama  lilivyokutwa eneo la Manyoni mkoani Singida likiwa limekatika katikati kutokana na kuelemewa na uzito wa mzigo lililoubeba.
-----------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtaka Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kuhakikisha kuwa Sheria ya Usalama Barabarani inasimamiwa vizuri ili kuhakikisha kuwa barabara zinazojengwa nchini zinadumu kwa muda uliokusudiwa.
 
Akizungumza katika eneo la Buziku mkoani Geita wakati akizindua ujenzi wa barabara ya Bwanga hadi Biharamulo yenye urefu wa kilometa 67, Rais Kikwete alisema kuwa wizara ya Ujenzi ni lazima ihakikishe inasimamia sheria zilizopo na hasa hii ya kutoruhusu magari yenye uzito uliozidi viwango vilivyoainishwa katika Sheria Namba 30 ya Mwaka 1973.

Akisistiza umuhimu wa kutunza barabara Rais Kikwete alibainisha kuwa “adui wakuu watatu wanao sababisha barabara kuharibika mapema ni; magari yanayobeba mizigo zaidi ya uzito uliowekwa kisheria, ujenzi duni usiozingatia viwango na kuachwa kwa maji kuzagaa barabarani”.
 
Wakati huo huo Rais Kikwete alielezea kufurahishwa kwa kuanza ujenzi wa mradi huo kwani wapo baadhi ya watu waliokuwa waliokuwa wakieneza taarifa kuwa sehemu hiyo ya barabara haiwezi kujengwa lakini sasa wameumbuka.

Awali akitoa maelezo ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Injinia Patrick Mfugale alielezea kuwa mradi mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegharimu Shilingi bilioni 55 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania. “Mradi huu utajengwa kwa muda wa miezi 27 na hivyo kukamilika mwezi Februari mwaka 2015” alisema Injinia Mfugale.

Naye Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Magufuli alimhakikishia Rais Kikwete kuwa wizara yake itahakikisha kuwa inamsimamia mjenzi wa mradi huo ambaye ni Kampuni ya Sinohydro Ltd. ya kutoka Jamhuri ya Watu wa China ili aukamilishe kwa muda na viwango vilivyokusudiwa na bila ya visingizio vya nyongeza ya gharama.

Akimpongeza Rais kwa kutekeleza ahadi yake, Waziri Magufuli alibainisha kuwa wananchi wa mikoa  ya Geita na Kagera wamefurahishwa sana kuona kuwa hatimaye barabara hiyo muhimu inajengwa kwani hiyo ndiyo sehemu pekee iliyokuwa imebaki ikiwa haina lami kwa barabara inayounganisha mikoa hiyo ya ziwa.

Wednesday, 6 November 2013

CHADEMA yapata pigo kufuatia kifo cha Ghafla cha Naibu Meya wake...!!

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, Vicent Remoy, kufariki ghafla jana.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Meya wa Manispaa hiyo, Jafary Michael (CHADEMA), alisema Remoy ambaye pia alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kiboriloni, zahanati ya Jafary iliyoko katikati ya mji wa Moshi.
  
“Ni kweli amefariki, na mimi nimepokea taarifa hiyo dakika 30 zilizopita, na kwa mujibu wa taarifa za awali, ni kwamba alienda kutizama afya yake hapo zahanati baada ya kuhisi kifua kuwa kizito wakati akiwa shambani kwake Msalanga,” alisema Michael.

Alisema mara ya mwisho kuzungumza naye kuhusu ugonjwa ilikuwa ni wakati wamesafiri kwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya mazungumzo na serikali ya nchi hiyo ambako alimwambia kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu (gauti).

Mstahiki Meya Michael ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Manispaa ya Moshi, alisema chama kimepokea kifo hicho kwa mshituko mkubwa kutokana na ukweli kwamba Remoy ndiye alikuwa muasisi wa chama katika Manispaa ya Moshi.
 
“CHADEMA manispaa tumepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha huyu mzee. Mbali ya kuwa muasisi wa chama, pia alikuwa kiungo muhimu kama mtu mzima kwa wanasiasa ambao ni vijana bila ya kujali itikadi za kisiasa,” alisema Michael.

Alisema pia marehemu alikuwa Diwani wa Kata ya Kiboriloni kwa vipindi vitatu mfululizo kuanzia mwaka 2000 hadi sasa, huku akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CHADEMA katika Manispaa ya Moshi.
 
“Naweza sema alikuwa ni kiongozi mwandamizi ndani ya CHADEMA, na pia ameshikilia nafasi ya naibu meya kwa vipindi vyote vitatu. Mara ya mwisho alichaguliwa kwa kura zote ambazo zilipigwa na madiwani wa CHADEMA na CCM,” alisema Michael.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na kwamba hadi sasa chanzo cha kifo chake hakijafahamika

Monday, 4 November 2013

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA DKT SENGONDO MVUNGI ALIYEJERUHIWA KWA MAPANGA NA MAJAMBAZI....

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia na daktari wa zamu wakimwangalia Mjumbe wa Tume ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI) jana Oktoba 3, 2013 kufuatia kujeruhiwa kwake na watu wanaosadikiwa ni majambazi usiku wa Jumamos Oktoba 2, 2013.(PICHA NA IKULU)

HATIMAYE MSAKO WABAINI MKOA WA ARUSHA KUONGOZA KWA KILIMO CHA BANGI HAPA NCHINI...!!


IMEBAINIKA kuwa Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi.

Akizungumzia ishu hiyo wakati wa uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Arumeru jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikemea vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku akisisitiza kula sahani moja na wahusika.

Kamanda huyo aliwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara moja wanapogundua uhalifu wa aina hiyo na mwingine

UNYAMA...!! MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AUAWA KINYAMA NA KUNG'OLEWA JICHO MOJA HUKO TARIME..!!


MWALIMU wa shule ya msingi Nyarero katika tarafa ya Inchage wilayani Tarime mkoani Mara, Joshua Makuri (34), amekutwa amekufa na mwili wake kutelekezwa katika maeneo ya uwanja wa shule ya msingi Turwa Tarime.
Katibu tarafa ya Inchage, Jonathan Machango, alisema jana kuwa mwili wa marehemu uligundulika mwishoni mwa wiki iliyopita na watu waliokuwa wakipita karibu na maeneo ya viwanja vya shule ya msingi Turwa.
Mwili huo kwa mujibu wa Machango, ulikutwa na majeraha ambapo jicho moja lilikuwa limetobolewa.
Machango alisema watu hao walipoona mwili huo, walitoa taarifa Polisi ambapo askari walifika na kuuchukua na baada ya muda ndugu za marehemu walijitokeza kuutambua katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa maalumu wa Tarime Rorya ACP, Sweetbelt Njewike, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na tukio hilo.
Mwalimu Makuri alikuwa akifundisha katika Shule ya Msingi Nyarero na mwili wake ulichukuliwa na ndugu zake kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika katika kijijini cha Nyarero.

---HABARI LEO