Thursday 5 December 2013

STRESS Vs ADDICTION

STRESS Vs ADDICTION
 
 
 
 
the stressful situation that is associated with increased intensity or persistence of distress—the greater the uncontrollability and unpredictability of the stressful situation, lower the sense of mastery or adaptability, and greater the magnitude of the stress response and risk for maladaptive behaviors such as drug addiction.

JE UNAFAHAMU FAIDA NA UMUHIMU WA TENDO LA NDOA KWA WANA NDOA...?? SOMA HAPA NIKUFAHAMISHE,,,,

Kuwepo na mapenzi ya dhati kati ya wanandoa hufanya mambo mengi kuwa rahisi na mepesi bila kujalisha ni kipindi cha furaha au majonzi; sababu inakuwa upo na mtu ambaye anakufanyia unafuu wa mhusika kuamini kuwa kila kitu hatimaye kitakuwa sawa mradi huyo mpenzi wako yupo karibu na wewe anakupenda na mnashirikiana vilivyo kwa kujaliana kwa misingi ya ‘Chake changu, changu chake’.  

Mapenzi na kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao hasa kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu.

Siri ya kufurahia tendo la ndoa ni wanandoa wote kuridhika na utendaji wa mwenza wao hasa wakati wa tukio, kwa kujituma, kuwa mbunifu, kutaka na kufurahia tendo hilo. Ingawa ni kweli kwa nadra inaweza tokea mwenzako akawa na hamu na wewe usiwe nayo (ikitokea mara chache sana – hili linaeleweka, na linaweza kukubalika ila si kwa kuzoea na ikawa utamaduni; iwe kwa mwanaume ama mwanamke) . 

Izingatiwe kuwa, kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi rahisi… Mazingira ya kufurahia tendo hili muhimu ni lazima yajengwe na yaimarishwe mara kwa mara. Maana ni wazi kuwa uhai wa kila ambalo linatakiwa kuishi ni lazima litunzwe kwa umakini na kujali. Hivyo kufurahia tendo la ndoa pia hupaswa kuimarishwa kwa nilivyotaja hapo awali – Kupenda, kujituma, utundu, maarifa na Ubunifu. Na haya yote huwa rahisi sana ikiwa mwanandoa wako wampenda ama kumkubali, na kubwa kuliko ikiwa na yeye pia hujituma, ‘ni mtundu’ na ana maarifa pia. 

Hivi vitu (Kujituma, utundu, maarifa na ubunifu) haviji hivi hivi pia… Na ndio kwa misingi hiyo wanandoa hushauriwa kuzungumzia tendo la ndoa, kama haridhiki katika tendo, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda, wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho kinakupandisha mzuka – huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo (TAHADHARI – Yapaswa kuwa na mipaka pia). 

Mnaweza msiwe kila mmoja si mtaalam kwa mwenzie mnapoanza mahusiano yenu ya mapenzi, ila inapaswa na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ufundi huo unaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kwa mwenza wake huyo na si kupungua. Izingatiwe pia kuwa, Kufanya mapenzi si lazima ukafanya kama vile ambavyo picha za ngono huonyesha ili kujua mnafurahia, msingi ni kutafuta rhyme ambayo huwafanya wote mfurahie tendo hilo la ndoa na kuwafanya kuwa na kiu juu ya mwenza wako pale unapokuwa umemkosa. 

Ndoa si kufanya tu Mapenzi ni zaidi ya hapo, ila mwisho wa siku kufanya Mapenzi ni muhimu mno kwa ustawi wa ndoa kati ya wanandoa. Ni suala ambalo kiharaka haraka linaweza chukuliwa kwa wepesi, ila mwisho wa siku lina faida sana. 


FAIDA YA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA

Linajenga ukaribu zaidi kwa wanandoa 
Tokana na majukumu ya kifamilia ambayo yanaenda yakikua kwa kasi na kufanya baadhi ya wanandoa kutokuwa na wakati wa kuwa karibu zaidi kunakuwa na muda mchache kwa baadhi kubadilishana mawazo. Wanandoa wengine wamefaulu kwa kuhakikisha kila siku/au mara kadhaa kwa juma kujulishana habari zao wanapokuwa hawapo pamoja. Tendo la ndoa linaweza tumika kama wakati muafaka wa kila mmoja kutiririka na kuongea mambo mbalimbali na hata kupanga mipango yenu ya kimaisha. Hilo hutokea pale mnapokuwa mnataka kujianda, nusu fainali au baada ya mchezo kuisha tegemeana na mtiririko wenu upo vipi. 
Black-couple-in-bed 

Kumwelewa Mwenzi wako 
Tendo la ndoa lina lugha yake… Tendo hili haliishi tu katika kufurahia na kufika kileleni bali pia linasaidia kumwelewa na kumsoma mwenzi wako. Ndio maana ni vema sana kumjulia mwenza wako kitabia na mwenendo kwa kuhusisha tendo hilo. Ikiwa wenza mna tabia ya kushirikiana na kuhusishana katika masuala ya kila siku ni rahisi kutambua kuwa mwenza wako siku hiyo kachoka, kachukizwa (iwe na wewe ama mtu mwingine), ana mawazo, ana wasiwasi, hana raha n.k. 
Haijalishi kuwa mwenza wako yupo katika hali ipi wengi hujitahidi hilo lisiwe kikwazo kwa tendo la ndoa (hasa wanaume) – Hivyo ni rahisi kumjulia tokana na namna mnavyokuwa faragha kujua kuna jambo ama la. Ni wazi wakati mwingine kunaweza kuwa na jambo na mwenzi wako asikuhusishe, kupitia tendo la ndoa unaweza pata viashiria. 

Inasaidia wanandoa kupata Watoto 
Watoto wana raha yake katika ndoa, na wana nafasi kubwa sana katika kuweza kuimarisha ndoa, kuleta furaha katika familia, kuwajenga na kuwa komaza kama wazazi na pia kuwaunganisha zaidi wanandoa kama mwili mmoja. Si wote wamejaaliwa kupata watoto (my heart goes out to them) – ila ukweli ni kuwa mara nyingi hiki ni kipengele muhimu katika ndoa ambacho wanandoa wenyewe na jamii hutarajia kuwa muhimu kufanikisha ili ndoa ionekane kuwa ina mafanikio. Niongeze kuwa tumepishana kutafsiri mafanikio ni nini katika ndoa, ila wengi huwa na msimamo wa kuwa watoto ni muhimu katika ndoa. 
sex-in-marriage 

Kutatua ugomvi/mgogoro kati ya wenza 
Ugomvi haukwepeki hata kama mwapendana vipi (ingawa frequency ya ugomvi hupishana kati ya wanandoa). Tendo la ndoa linazungumza mambo mengi sana…. Kitendo cha kukutana kimwili na mwenza wako kwa namna moja wapo inakuwa ni akili na mwili wako kukubali kuwa umejitoa kwa mwenzi wako kwa wakati huo. Kuna makabila ambayo hata uwe umegombana vipi na mke/mume wako, ikitokea tu ukalala naye na kufanya tendo la ndoa haijalishi kosa lilikuwa ni lipi inachukuliwa limesamehewa na yapaswa kusahau na kusonga mbele. 

Kupunguza uchovu/Msongo wa mawazo 
Ndoa ni moja ya njia kwa baadhi kuweza kupunguza uchovu alio nao na kwa wengine hata msongo wa mawazo. Tendo likifanywa vema na kwa ustadi, huweza kumwondolea mwenzi wako uchovu au msongo wa mawazo kwa kiwango kikubwa. Unafuu huo utegemea lakini, wengine inakuwa tu unafuu wakati wa tendo hilo na hali wengine hupata nafuu ya muda mrefu.  Hivyo ikiwa mwenzi wako yupo katika hali hiyo katika kutafuta namna ya kuhakikisha anapata unafuu, unaweza tumia tendo la ndoa kama silaha ya kumrudisha mwenzi wako katika hali nzuri. 

Linajenga heshima ndani ya ndoa (hasa kwa wanaume) 
Hili linawezekana pande zote (mke na mume) mmelipa umuhimu wa pekee tendo la ndoa hadi mkiwa faragha wote hufurahia tendo hili hadi kuna wakati mwajihisi mpo mwili mmoja kama si ndani ya ngozi moja. Tunarudi palepale, kuwa ni muhimu ukampenda mtu wako, ukapenda hilo tendo, mengine yanafuata mkiwa faraghani. 

Linatumika kupata unachotaka/Kulaghai (hasa kwa wanawake) 
black-love 
Hili linategemea unalifanya kwa namna ipi… Ukilifanya kana kwamba ni hongo ya lazima na kuwa wamaanisha hutokubali kuwa faragha bila kutimiziwa kitu Fulani – Hapo inakuwa ni tatizo na ndio ulaghai wenyewe. Ila lifanywapo kwa upendo, utani wa kimapenzi, kwa kutoa maneno matamu na kubembembeleza, husaidia kuongeza ashiki kwa wapenzi (inaweza isiwe kwa wote) na huku pia ukifanikiwa kupata kile ambacho unataka mwenzio akiwa katika mood nzuri. 

kipanya-artwork 
Wapendwa nakaribisha mawazo, michango, maswali, na maoni toka kwenu

BAADA YA SHULE KUFUNGWA MWALIMU WA SEKONDARI AMUA KUUZA KAHAWA MTAANI...!!

    
Hivi ndivyo Mnyetishaji wetu alivyomnasa ticha huyu wa sekondari mkoani Dodoma akiuza kahawa mtaani ili kujinusuru na ukata wa maisha magumu ya kitaa, 

''Leta chikompe kyako nkupe kyai kya mata na kyai kya kapyaru...au kiguuju'' tcha jimmy:
  Pia mwalimu huyo pamoja na shughuli zote za uwalimu na kuuza kahawa pia na msanii anayefanya vizuri kwenye Game la music husasani mkoa wa Dodoma,



"Propaganda zinazoendelea sasa hivi zinatuimarisha CHADEMA"......Dk. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.

Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.


Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.

Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.

Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.

“Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito,” alisema.
Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

“Mimi nawaambia watulie tu… Nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya CHADEMA hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.

“Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na CCM, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.

“Wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia Watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya Watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza,” alisema.

Dk. Slaa alisema kuwa CCM wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na CHADEMA, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.
Safari yapata matatizo.

Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha Dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.

Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.

MIZENGO PINDA:MSHAHARA WANGU KAMA WAZIRI HAUZIDI SH MILION 6..

Waziri Mkuu amedai bungeni muda huu kwamba mshahara wake hauzidi Tsh. 6mil na akadai wanaodai analipwa zaidi ya hapo ni uzushi mkubwa kiasi kwamba yeye ni mkopaji tu katika mabenki na kuwa mshahara huo ni pamoja na mapato ya mkewe.

Source: Leo Bungeni -TBC