Miongoni
wa makundi ya vijana hasa wenye umri wa kati miaka 15-23 wengi wao
huota wakifanya mapenzi ndotoni, lakini mbali na hao kuna watu wazima
pia ambao hukumbwa na tukio hili. Uotaji wa ndoto hii umekuwa
ukitafsiriwa na wengi kwa maana tofauti tofauti, huku wengine
wakiuhusisha na ufanyaji mapenzi na Majini.
Uchunguzi unaonyesha kuwa uotaji ndoto za kimapenzi huwatokea hata watu
ambao hawajawahi kufanya kitendo hicho kabisa, huku watu wanaofanya nao
wakiwa ni wale wanaowafahamu kwa sura au wasiowafahamu. Wengi wamekuwa
wakijiuliza maswali mengi juu ya nini kinachangia uotaji huu wa ndoto za
kimapenzi?
Kitaalamu ndoto hizi hutokana na mawazo ya mtu husika ambayo yanaweza
kugawanywa katika sehemu mbili ambazo ni MAWAZO YALIYO WAZI au
YALIYOJIFICHA. Mtaalamu wa masuala ya ndoto Daktari Gillian Holloway
anaeleza kuwa ndoto hizi hufumbua maamuzi na hisia zilizojificha nyuma
ya ubongo.
Pamoja na tendo hili kuwa baya katika mitazamo ya wengi hasa kiimani,
lakini bado si kitaalamu halina ubaya kwa kiwango hicho kwani mara
nyingine husaidia kutafsiri yale ambayo wahusika hawakupata kuyafahamu
kabla. Kwa mfano vijana ambao hawajafanya mapenzi hupata kutambua raha
itokanayo na kitendo hicho na hivyo kuwaamshia hisia za kimapenzi ambazo
pengine hawakuwa nazo hapo awali.
Wachunguzi wa masuala ya ndoto wanasema ndoto hizi zikitumika vizuri
zinaweza kusaidia kumpata mchumba anayegusa hisia za moyo, aina ya
mapenzi yanayokufurahisha, haiba ya mpenzi umpendaye na wakati mwingine
huchangia kuongeza uzalishaji wa homoni na kupunguza msongo wa mawazo
sawa na mtu aliyefanya mapenzi laivu.
Hata hivyo watu wanaotajwa kutokewa na kitendo hicho mara kwa mara ni
wenye tabia ya kuogopa wanaume/wanawake na hivyo kuzikandamiza hisia
zao, pamoja na wale wanaochochea hamasa za kingono na kutokuzikata,
(mfano kufanya romance na kuachana bila kuingiliana), wanaotazama picha
za ngono, wanaozungumzia sana mambo ya kimapenzi na wale wanaowaza sana
wapenzi wao walio mbali.
Kwa maana hiyo ili mtu asiweze kutokewa na ndoto hizo hana budi kujizuia
na mambo hayo yanayotokana na uamshaji na ukandamizaji wa hisia za
kingono. Hii ina maana ya utashi wa mtu wa kutopenda kuota, lakini si
kwamantiki kuwa uotaji huu unauhusiano na mambo ya kishirikina au
kichawi kama ambavyo watu wengine wanavyoaminishwa.
Mwisho kama kuna wanaodhani kuwa ndoto hizi zimewadhuru kwa namna moja
au nyingine, wafahamu kuwa kilichowadhuru si kuota ndoto hizo bali ni
wasiwasi wao unaotokana na kusikia na wala si madhara kwa maana ya kuota
kwenyewe, kwani ikiwa ni ndoto hata wanyama kama Mbwa, Paka na Sungura
nao huota wakifanya mapenzi, ushahidi ambao unatosha kutupilia mbali
hoja ya ndoto kutokana na majini
Kumbe imani potofu tu ndio imewajaa watu
ReplyDelete