'Panya mwokozi wa maisha'
Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza
kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya
hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio
Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa.
Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo
inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.
Uwezo kutokana na maumbile ya pua
Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu
vyenye madini ya milipuko.Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza
panya kwenye chuo cha Sokoine,Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza
zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji. Kabla ya panya
kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza
viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.
Kutafuta hatua kwa hatua
Panya hujifunza kufuta eneo fulani hatua kwa hatua. Waya au kamba
hufungwa mwilini kutoka kwenye ufito.
Wasimamizi wawili husimama kila upande wa ufito na kumruhusu panya
kutembea toka mwanzo wa ufito hadi upande mwingine kwa kufuata jinsi
waya au kamba alizo fungwa mwilini.
Katika mafunzo ya awali panya hufunzwa kunusa kemikali aina ya TNT ndani
ya chombo cha chuma.
Kugundua mabomu ardhini
Baadaye kila panya hufanya mafunzo kwenye eneo ambalo kuna mabomu ya
ardhini yaliyofukiwa na vifaa ambayo huzuia mlipuko.
Ikiwa panya ameweza kunusa na kutambua yalipo madini asilia ya TNT huwa
anasimama na kuanza kufukua sehemu hiyo ya ardhi iliyofukiwa bomu.
Kuwafundisha panya kunachukua muda wa mwaka na inagharimu dola za
Kimarekani $6,000 sawa na Euro 4,670.
Zawadi kwa ufanisi
Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti
maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama
zawadi.
Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa
siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza
kugundua wapi kumefukiwa bomu.
Pua za kunyumbulika
Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani
hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha
kama walivyo mbwa. Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata
kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na
mtu yeyote. Hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda
kufanya kazi Msumbiji, Angola,Thailand na Kambodia.
0 comments:
Post a Comment