Tuesday, 26 November 2013

YAJUE MAAJABU YA BROKOLI

Hii ni aina fulani ya mboga ya majani, iko kama maua ya maboga au uyoga, inapatikana katika masoko mengi makubwa nchini. Brokolini huwa na kiasi kingi cha kirutubisho aina ya ‘sulforaphane’ ambacho uwezo wake wa kutoa kinga ni mkubwa kwa magonjwa mengi. Inatoa kinga dhidi ya saratani ya matiti, ini, mapafu, kibofu, ngozi, tumbo na kizazi.
broko
Vilevile brokoli ina uwezo wa kupunguza/kukata mafuta katika mwili ambayo huweza kusababisha magonjwa kama ya kisukari, shinikizo la damu na kadhalika. Faiba ambazo hupatikana kwenye brokoli zinasaidia kemikali ambazo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Faiba hizi husaidia katika kutolewa kwa kemikali hizi.
Brokooli pia husaidia katika kupunguza sumu mwilini. Wachambuzi wamegundua kua brokoli ina mchanganyiko wa Glucoraphanin, gluconasturtiian, na glucobrassicin ambao una uwezo wa kufanya hatu zote za kusawazisha, kupunguza na kutoa kabisa sumu ambazo zina madhara ndani ya mwili wa binadamu.
Brokoli ina uwezo wa kusaidia mtu mwenye upungufu wa Vitamin D, A na K mwilini. Kwa watu ambao wanahitaji kupata Vitamin hizi, wanashauriwa kujumuisha mboga ya brokoli katika mlo.
Vitamin D na Kasiam (Calcium) inayopatikana katika brokoli husaidia kuongeza afya ya mifupa katika mwili wa binadam.

Namna ya Kutengeneza Brokoli
Brokoli inahitaji kuliwa na virutubisho vingi zaidi ila kufanikisha kazi yake mwilini. Kwanza kabisa chukua brokoli zako, ziweke kwenye bakuli kisha zioshe. Ukishamaliza kuziosha. Chemsha maji katika sufuria.
Cha kwanza kabisa, zikate brokoli katika vipande vipande kama picha inavyoonyeha apo chini:
broko 2

Yakishachemka, ingiza brokoli zako na ziache kwa mda wa dakika 2-3. Baada ya hapo brokoli zako zipo tayari kwa kuliwa na chakula chako.

0 comments:

Post a Comment