Wapiganaji
wa Kiislamu wa Al Shabaab nchini Somali wamesema wao ndio waliotekeleza
shambulizi la bomu la kujitoa muhanga nje ya hoteli katika mji mkuu wa
Mogadishu nchini Somalia ambapo watu sita waliuawa wakiwemo maafisa wa
polisi.
Kundi hilo la Al Shabaab ambalo lilifurushwa na majeshi ya Somalia yakishirikiana na yale ya Umoja wa Mataifa AMISOM miaka miwili iliyopita wameapa kuendeleza harakati zao za kufanya mashambulizi.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya ndani wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia BBC kuwa watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kujitoa muhanga.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Adan ambaye yupo Mogadishu amesema sauti ya mlipuko ulisikika katikati ya mji huo wa Mogadishu.
0 comments:
Post a Comment