Unaweza
kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida
kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari
yaliyoshindikana hospitalini.
Kwa
mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za
kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi
ama zilizokaangwa:
HUIMARISHA MOYO, MIFUPA
Mbegu
za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya
Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa
ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa
kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi.
KINGA YA MWILI
Mbegu
za maboga zina kiwango kingi cha madini aina ya Zinc, ambayo yana faida
nyingi mwilini, zikiwemo uimarishaji wa kinga mwilini, ukuaji wa seli,
macho na ngozi ya mwili. Vile vile Zinc huimarisha nguvu za kiume.
SARATANI YA KIBOFU
Kutokana
na kuwa na kiwango kingi cha Zinc, utafiti umeonesha kuwa mafuta na
mbegu zenyewe za mabogo huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya
kibofu.
KINGA YA KISUKARI
Utafiti
umeonesha pia kuwa mbegu za maboga huweza kuimarisha utokaji wa
‘insulin’ mwilini, hivyo kuwa kinga au kuleta ahueni kubwa kwa wagonjwa
wa kisukari.
TIBA KWA WALIOFIKIA UKOMO
Mafuta
ya mbegu za maboga hayana madhara, zaidi yana kirutubisho muhimu cha
kurekebisha Cholesterol mwilini, kushusha shinikizo la damu, kuzuia
uvimbe, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo vya mwili na vile vile
huondoa maumivu mbalimbali yanayowapata wanawake wenye umri mkubwa
waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause).
UGONJWA WA INI
Mbegu
za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa
nyemelezi. Mbali na hayo, mbegu zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi
ya magonjwa ya ini na moyo.
USINGIZI
Kwa
watu wenye matatizo ya usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja
na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha
kuwa mbegu za maboga zina kirutubisho kinachochea uzalishaji wa homoni
za usingizi kwa wingi.
UVIMBE
Mbegu
za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia
magonjwa yote ya uvimbe mwilini, yakiwemo ya kuvimba miguu, vidole na
hata majipu.
JINSI YA KULA MBEGU
Hakikisha
unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizosafi ambazo hazijakaa muda
mrefu. Kwa usalama zaidi, zioshe kwa maji safi kisha zianike, inapendeza
zaidi ukila bila kukaanga, lakini pia ukiamua kula za kukaanga bado
utapata faida zake, muhimu usiziunguze wakati wa kukaanga. Kwa kawaida
hukaangwa kwa muda usiozidi dakika 10 tu.
Friday, 29 November 2013
AFYA JE...?? UNAFAHAMU FAIDA ZA KULA MBEGU ZA MABOGA....?? SOMA HAPA NIKUJUZE...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment