Zaidi
ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo
kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo
ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji
huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na
Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa,
kulawitiwa na kubakwa.
Mtoto
Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo
iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert
(8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo
mwishoni mwa wiki.
Watoto
hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati
wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23
mwaka huu.
Wakiwa
wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha
Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna
watoto wengi wa kike na kiume.
Walisem
a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo,
kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao
ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.
"Jumba
hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na
nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo
kupanda na kushuka kilima.
"Tunapigwa
fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa
zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na
kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa
uchungu akitokwa na machozi.
Aliongeza
kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea
kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja
aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na
kuacha mlango wazi.
"Hali
hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache
waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu
ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.
"Watoto
wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza
kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini
kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana
hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema
Emmanuel
Aliongeza
kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali
waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo
vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.
"Tulipanda
gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na
Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa
tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo
alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.
"Tulitembea
kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara
kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na
kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu
kwa siku.
"Tulikula
saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia
sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba
kokoto ikiniita.
"Nilidhani
naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa
namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo
tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na
kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.
Akizungumza
na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake,
walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba
hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama
mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za
mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya
Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao
bila mafanikio.
"Nimepoteza
fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika
kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika
Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.
Alisema
zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana
baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na
kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi
linalowateka watoto na kuwatesa.
Kamanda
wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.
Alisema
makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya
kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo
hilo watoe ushirikiano.
-Gazeti la Majira.
0 comments:
Post a Comment