MWANAMKE
anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za
kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza
mwili wake.Maumivu kwenye matiti:
Hii
ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini
huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi
wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo
kawaida.
Maumivu mwilini:
Utaanza
kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida
hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha
mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na
kusababisha maumivu hayo.
Kutokwa damu bila kutegemea:
"Wanawake
wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku
zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba
asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist.
Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au
inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya
kipimo cha ujauzito..
Kuchoka:
Unapojisikia
kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini,
lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi
kipya cha mabadiliko.
“Tambua
kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto
tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na
usingizi” anasema Goist.
Chuchu kuwa nyeusi:
Chuchu
huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli)
kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema:
“Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda
wa kama wiki kumi zipite.”
Kichefuchefu:
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba:
Kuna
wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia
kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula
kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako
haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na
kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo mara kwa mara:
Kwenda
haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya
kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti
zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito,
ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya
kufanya kazi kwa muda mrefu.
Tamaa ya vitu mbalimbali:
Kutokana
na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo
humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko
yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani
au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuumwa kichwa:
Kuongezeka
kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani
katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili
unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Kufunga choo:
Homoni
ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana
na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii
inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Kuwa na hasira
"Kutokana
na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo
itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
Kuongezeka kwa joto mwilini:
Kipimo
cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa
kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa
linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa
inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
Friday, 29 November 2013
KWA WANAWAKE: FAHAMU DALILI KUMI ZA AWALI ZA KUGUNDUA KAMA UNA UJAUZITO (MIMBA)...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment