Monday, 11 November 2013

MAISHA YA WATU MILLIONI 800 HATARINI, soma hapa upate kufahamu

Utafiti uliofanywa na wanasayansi umeonyesha kuwa kuchafuliwa kwa bahari ni athari za mabadiliko ya tabia nchi na ni kitisho kwa viumbe vya baharini.
Matokeo ya utafiti huo yaliyofanywa na wanasayansi 29 kutoka nchi 10 yametathimini pia kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya watu zaidi bilioni 2 wanaoishi kando ya bahari na ambao wanategemea kipato kinachotoka na shughuli wanazofanya baharini.
Kwa mujibu wa mtafiti na masuala ya elimu ya uhusiano wa viumbe na mazingira katika chuo kikuu cha Hawai huko Honolulu, Camilo Mora utafiti huo umebaini kuwa moshi unaotoka viwandani unachangia bahari kuwa na joto kali zaidi na kubadilika kuwa tindikali na hivyo kupunguza kiasi cha hewa safi katika maji ya bahari, mabadiliko ambayo yanakuja mara moja na haraka na kuharibu viumbe vya baharini.
Asilimia 70 ya eneo la bahari kutotumiwa
Mtafiti huyo ameliambia shirika la habari la IPS kuwa hadi kufikia mwaka 2100 asilimia 70 ya eneo la baharini halitafaa kwa matumizi.
Utafiti huo umetathimini hali ya sasa na ya baadaye ya moshi unaotoka viwandani utakavyoathiri viumbe vya habarini kama vile samaki, makaa ya mawe, wanyama wa baharini, mimea na viumbe vinginevyo.
Mvuvi akitoka kuvua samaki baharini. Mabadiliko ya tabianchi yameelezwa kuathiri upatikanaji wa chakula na hivyo kuyaweka hatarini maisha ya mamilioni. Mvuvi akitoka kuvua samaki baharini. Mabadiliko ya tabia nchi yameelezwa kuathiri upatikanaji wa samaki
Kwa upande wake mtafiti kutoka taasisi ya kimataifa ya utaifiti iliyopo Stavanger nchini Norway, Andrew Sweetman amasema ni wakati sasa wa kuangalia na kukabiliana na hali hiyo kutokana na ukweli kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi yataanzia kwenye ukanda wa bahari kuelekea nchi kavu.
Uhaba wa chakula pia kuathiri wengi
Kati ya watu milioni 500 hadi 870 maskini duniani kote wapo hatari kukosa chakula na mapato kutoka habarini kutokana na athari hizo.
Wanasayansi hao wameeleza kuwa kuna athari nyingi zaidi zinazosababisha kupungua kwa viumbe baharini kama vile uvuvi holela, matumizi ya kemikali za sumu na uchafuzi wa bahari lakini utafiti huo ulilenga zaidi namna mabadiliko ya tabia nchi yatakavyoathiri viumbe vya baharini.
Hali ambayo amesema kuwa inaashiria namna watu wanavyovua samaki na viumbe vingine vya baharini kwa wingi zaidi ya kiwango kilichopo. China, Taiwan, Urusi, India na Japan zimetajwa kuongoza kwa uvuvi holela wa samaki duniani.
Uvuaji kupita kiasi wa samaki ni chanzo cha kupungua kwa samaki baharini. Uvuaji kupita kiasi wa samaki ni chanzo cha kupungua kwa samaki baharini.
Alex Rogers mwanasayansi kutoka chuo kikuu cha Oxford Uingereza amesema dunina inashuhudia mabadiliko ya haraka yanayotokea na kuathiri viumbe vya baharini lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa inapaswa kutambua kwamba hali hii ikiongezeka italeta gharama kubwa hapo baadaye.
Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha elimu ya sayansi baharini, Elizabeth Selig ametoa wito kufanyika juhudi za haraka kuokoa viumbe vya baharini kutokana na umuhimu wake kiuchumi lakini pia kiafya

0 comments:

Post a Comment