Saturday, 16 November 2013

MENO YA TEMBO YAWAPELEKA JELA MIAKA 70

MENO YA TEMBO YAWAPELEKA JELA MIAKA 70
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, katika Mkoa wa Katavi, imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka 70 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya Sh45 milioni.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na ule wa upande wa utetezi.
Waliohukumiwa kifungo hicho ni, Gwabi Mayala(39 mkazi wa Kijiji cha Majimoto katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
tembo
Mayala alikuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo na amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa fidia ya Sh. 45 milioni/=. Wengine waliohukumiwa ni Mashaka Mabanga (33) mkazi wa Sumbawanga katika Mkoa wa Rukwa na Adamu Kalinzi (30) mkazi wa Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele ambao kila mmoja amehukumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Mapema, Mwanasheria wa Serikali katika Mkoa wa Katavi, Fadhili Mwandoloma, alidai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo usiku wa Oktoba 10 mwaka huu katika Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele

0 comments:

Post a Comment