Niliwahi kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata
watatumia kwenye nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na
kununua gari huku wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.
Sasa basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa
kufanya mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha
pesa kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya
inch 85 na usirudishiwe chenchi.
tovuti hii ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii
ina vitu vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na
sura kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya
kutumia remote.
Smart
contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyinginembalimbali ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati mmoja.
Ina music system yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna
haja ya kununua home theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila
decorder na ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo
unaiweka kwenye smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
0 comments:
Post a Comment