Tatizo la kutokwa na chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu za usoni na kuharibu sura ya mwanadamu hasa wanawake.
Ugonjwa huu umekuwa ukiwachukiza baadhi ya wanawake na wanaume kutokana na kuharibika kwa uso wao na matokeo yake kujikuta wakienda kununua vipodozi vyenye kemikali kali ambazo ni hatari kwa afya ya ngozi zao.
Vipodozi hivyo ni hatari kwani vingine huweza kuchubua na kusababisha ngozi kukosa kinga,hivyo kuleta madhara makubwa mwilini.
Chunusi huwatoka na kuwasumbua watu wengi hasa vijana wenye umri wa kubalehe lakini pia hushambulia hata watu wazima.
Ukitokwa na chunusi maana yake una mchanganyiko wa magonjwa tofauti ya ngozi sehemu za usoni kwani vipele vidogo vinavyotoka husababisha maumivu na muwasho kwa muathirika.
Vipele hivyo baadaye hutunga usaha na kuwa chunusi ngumu.
Kitaalamu ili mtu awe na chunusi kuna vijidudu hushambulia vitezi vya ngozi ya uso vijulikanavyo kwa jina la Pilosebaceous na Sebaceous gland.
Tezi hizi hutoa mafuta mengi usoni na yakizidi huwa chakula cha vijidudu (bacteria)wanaokaa kwenye ngozi na kusababisha uingiaji wa vidudu hivyo kwenye hizo tezi na kusababisha chunusi.
Chunusi hutokea baada ya tezi za Pilosebaceous kuziba (obstruction), huzibwa na mgando wa mafuta ya usoni na kusababisha wadudu kuingia kwenye tezi za usoni ambapo wadudu hao hushambulia ngozi ya usoni.

Chunusi
ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo
vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea
wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta
au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio
ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano
nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..
Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .
Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .
Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata
chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka
ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza
kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi
ni dalili ya balehe.
Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya
binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na
kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia
kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.
Wakati
wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati
huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa
hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa
mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na
seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta
uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto.
Maambukizi
zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia
vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple
hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za
damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho
vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita
chunusi.
Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko
nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au
vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali
hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli
mpya kutengenezwa.
Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali
hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho
baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega
na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous
nyingi.
CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
1. UMRI
– Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu
anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta
(sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2. VIPODOZI
–Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina
mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
4. DAWA-Chunusi
zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile
antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na
tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu
ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili
kuongeza unene wa misuli yao.
5. MAGONJWA-
Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders)
huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
6. MAZINGIRA-
Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye
mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya
joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
9. HOMONI-
Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku
zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata
chunusi.
10. USAFI
WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na
kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka
zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu
wa kupata chunusi
11. MAWAZO
AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa
mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi
DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.
Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana

Daktari
kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu
akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya
chunusi.
Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

MATIBABU
Matibabu
ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa
seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.
Matibabu
huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la
kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama
nilivyoeleza hapo juu.
DAWA ZA KUPAKA
Kuna
dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa
chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu.
Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa.
Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa
nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo
vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa
seli mpya za ngozi
Dawa
hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku
hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha
kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa
kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile
Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T
(clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin
(minocycline hydrochloride) na
”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”
Wanawake
wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile
baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa
ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu
ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.
MATIBABU MENGINE
Kwa
nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin
grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na
kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi
na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa
baka.
MATIBABU MBADALA
Haya
hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na
kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu
nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu
wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini
ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na
Chromium.
Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
MUHIMU
Chunusi
haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu
60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona
haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza
kujitokeza unapoacha kutumia dawa.
Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
1. Osha
taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau
mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au
kitu choichote kigumu.
2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
7. Punguza mawazo
0 comments:
Post a Comment