Friday, 15 November 2013

HAYA NDIYO MATESO YA MAREHEMU DK. MVUNGI....

HADI anakata roho Novemba 12, mwaka huu, Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi amepitia mateso makubwa.

 

Dk. Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Novemba 3, mwaka huu alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani nyumbani kwake Kibamba-Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi).

Tangu lilipotokea tukio hilo, Dk.Mvungi aliishi katika mateso makubwa kutokana na kupoteza fahamu huku akipumua kwa kutumia mipira ya gesi hadi kifo kilipomfika katika Hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini.

 

Dk. Mvungi enzi za uhai wake.
Kwa takribani siku tisa, Dk. Mvungi alikuwa akisikilizia maumivu makali ya majeraha makubwa ya mapanga hivyo ni dhahiri kuwa alipitia mateso makubwa.

Watu kumi akiwemo John Mayunga ambaye ni mtuhumiwa wanaodaiwa kuvamia nyumbani kwa Dk. Mvungi wanashikiliwa na jeshi la polisi jijini Dar kwa ajili ya mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.
Watu hao walikamatwa wakiwa na mapanga pamoja na simu ya marehemu.

0 comments:

Post a Comment