likua
ni mwezi november tarehe 26 mwaka 2012 majira ya sa 2 usiku ndipo
ziliposambaa taarifa za kifo cha muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi
kipya ‘Bongo Fleva’ Husein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’.
Leo
tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya kumkumbuku
ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga.
wanafunzi wa madrasa wakiimba kaswida kwenye mkesha huu wa kumuombea marehemu Sharo Milionea
Jana
tarehe 25 november kulikua na mkesha maalum,Mkesha huu umeambatana na
kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa madrasa,Miongoni mwa watu
waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki
mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
Mama mzazi wa sharo milionea katikati ya kitale na rafiki wa kitale
millardayo.com
imepiga exclusive interview na mama mzazi wa Sharo Milionea pamoja
Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea ikiwemo
mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel,Azam pamoja na movie
ambazo aliziacha marehemu sharo.
‘Dhumuni
la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua ili
mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka sasa
mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa jumla
ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi rambi zao
nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake
kilichokua bunju alichotafutiwa na mjomba wake,nikamwambia mjomba wake
akiuze kwa sababu ya usumbufu maana mi nipo mbali huku,maana nilikua
kila siku nasikia mara wamekichota’.
‘Kuhusu
Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa marehemu kwa
hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli Mudy Suma kaliuza
lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua
katika vitu walivyonambia rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na
hiki ni pamoja na movie kwa hiyo movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa
ni movie moja ambayo amecheza yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo
Tuesday, 26 November 2013
TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI JANA KATIKA MKESHA WAKUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment