JESHI la Polisi limempa ulinzi wa siri Mbunge wa Kigoma
Kaskazini,Zitto Kabwe (CHADEMA) kama njia ya kumkinga asidhuriwe na
maadui wake katika siasa.
Hatua hiyo ya polisi imechukuliwa siku chache baada ya mwanasiasa
huyo kijana na mama yake mzazi, Shida Salum, kwa nyakati tofauti, kudai
kuwa Zitto amekuwa akiwindwa na watu ambao wamekuwa wakitishia uhai wa
wake kutokana na siasa zinazoendelea ndani ya Chadema.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kiliiambia RAI
kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao wiki iliyopita, baada ya jeshi
hilo kupata taarifa za tishio la kudhuriwa kwa kiongozi huyo kwa kile
kilichoelezwa kuwa tofauti baina yake na viongozi wenzake wa Chadema.
Kikao hicho ambacho kiliwahusisha makamishna kutoka makao makuu ya
jeshi hilo, kilipitia kwa kina taarifa ya kutaka kudhuriwa kwa Zitto kwa
kutofautiana msimamo na viongozi wenzake ndani ya chama hicho.
“Kikao kilifanyika Novemba 11 mwaka huu ambako pamoja na mambo
mengine kimeweza kujadili kwa kina kutaka kudhuriwa Zitto … hivyo
walitumwa makachero wa jeshi la polisi waweze kubaini anapoishi.
“Wamefanya kazi hii na sasa kiongozi huyo analindwa kuanzia nyumbani
kwake Tabata. Askari maalumu wamepewa kazi ya kuimarisha ulinzi nyumbani
kwake hadi katika nyendo zake,” kilisema chanzo hicho ndani ya jeshi la
polisi.
Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, kwa muda mrefu
amekuwa akitofautiana na viongozi wenzake hasa katika masuala ya taifa
hali inayofanya atafsiriwe kuwa anatumika kutaka kuivuruga Chadema.
RAI ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso
kupata uthibitisho wa uamuzi huo lakini alisema suala hilo liko mikononi
mwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
“Kwa jambo hili nakuomba mtafute Kamanda wa Mkoa husika, yeye anaweza
kukupa maelezo ya kina ya jambo hilo ndugu yangu au Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,” alisema Senso.
KOVA
Alipotafutwa jana, Kova alisema hawezi kukubali au kukata kwa sababu
suala hilo liko katika mamlaka ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi.
“Siwezi kusema ndiyo au hapana, nakuomba umtafute kamanda wa mkoa husika atakupatia maelezo ya kina,”alisema Kamanda Kova.
KAMANDA WA ILALA
Kamanda Minangi alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo, naye
alimrushia mpira Kova akisema ndiye pekee anayeweza kutoa ufafanuzi wa
suala hilo.
“Jamani nawaomba suala hili mmtafute Kamanda Kova ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi,”alisema Kamanda Minangi.
Kwa muda mrefu sasa, Zitto amekuwa akishutumiwa na viongozi wenzake
wa ngazi za juu katika Chadema akidaiwa kutengeneza ufa baina yake na
wazito ndani ya chama hicho tangu mwaka 2009.
Zitto amekwisha kuwahi kutangaza uamuzi wa kutaka kuwania uenyekiti
wa chama hicho aweze kupambana na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
Hata hivyo baadaye alijiondoa kuwania nafasi hiyo baada ya wazee wa
chama hicho kuingilia kati na kumsihi atumie busara kutogombea.
Katika siku za hivi karibuni, Zitto amejikuta akihusishwa na kile
kinachotajwa kuwa nyuma ya `usaliti’ unaodaiwa kufanywa na Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Arusha aliyesimamishwa, Samson Mwigamba.
Hata hivyo, Zitto alikanusha tuhuma hizo na kuwataka viongozi wenzake
kuelekeza nguvu kwa wanachama akisema malumbano hayatakijenga chama.
Mbali na hilo, kwa muda mrefu Zitto amekuwa na msuguano wa ndani na nje ya chama, hasa kutokana na misimamo yake.
Hivi karibuni, Mbunge Arusha Godbless Lema (Chadema) aliibuka na
kumtuhumu Zitto kwa uamuzi wake wa kutochukua posho za vikao bungeni
tofauti na msimamo alioutoa mwaka 2011.
Msuguano mwingine ni baina yake na vyama vya siasa kwa msimamo wake
wa kutaka vyama vyenye wabunge ambavyo vinapata ruzuku ya serikali,
viwasilishe ripoti ya ukaguzi wa hesabu zake kwa Msajili wa Vyama vya
Siasa.
Zitto ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC) pia aliwaonya viongozi wenzake kuacha propaganda kwa kulichukulia
suala hilo kuwa ni la siasa au lake binafsi.
Alisema anachokifanya ni kusimamia sheria kutokana na nafasi yake kama mwenyekiti wa PAC.
Vyama vya siasa vinatajwa kuchukua ruzuku ya Sh bilioni 67.7, lakini havijaanika mchanganuo wa matumizi yake.
ATUA POLISI
Katika hatua nyingine, jana Zitto alisambaza ujumbe kwenye mtandao
wake wa jamii akisema amelazimka kwenda makao makuu ya jeshi la polisi
kutoa maelezo kwa kutishiwa kifo.
Katika ujumbe huo alindika: “Nimetoka makao makuu ya upelelezi
kuandika maelezo kuhusu vitisho dhidi yangu, kufuatia hekaya inayoitwa
ripoti ya siri ya Zitto Kabwe.
“Chanzo cha hekaya ya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya
Chadema na kuwa ni Usalama wa Taifa au Chama Cha Mapinduzi (CCM)”.
Taarifa hiyo ilisema wahusika wanaendelea kuhamisha chanzo, lakini
wanaopaswa kujua watasakwa, kukamatwa na kuburuzwa mahakamani.
“Nimewashtaki kwa kunitishia maisha, ninawashtaki kwa kunichafua kwa
tuhuma za uongo, nafanya haya kwa lengo la kuhakikisha siasa za
kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa,”ilisema taarifa
hiyo.
MSIMAMO WAKE
Mwanasiasa huyo kijana ambaye amejipambanua kuwa mtetezi wa misingi
ya utaifa, raslimali za nchi, uchumi na masuala ya utawala bora ndani na
nje ya chama chake, alitoa msimamo wake kwa mara ya kwanza wiki
iliyopita alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa
Kolimba wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora.
“Katika umri huu mdogo, nimepigwa mishale mingi ya siasa, mimi ni
binadamu nina damu, nikipigwa hii mishale damu inatoka, ninaumia, sasa
nimechoka kupigwa mishale, lazima sasa tuambiane ukweli,” alisema Zitto.
Saa kadhaa baada ya hotuba yake hiyo, alisambaza tamko la maandishi ambalo lilibeba ujumbe unaofanana na ule alioutoa Kaliua.
Awali katika mkutano wa Kaliua, Zitto alisema alikuwa hayuko tayari
kuendelea kukaa kimya pasipo kuchukua hatua zikiwamo za sheria wakati
akichafuliwa.
Alisema alikuwa ameshamwandikia barua Katibu Mkuu wake, Dk. Willbrod
Slaa akihoji iwapo taarifa ya kumchafua iliyosambazwa katika mitandao ya
intaneti chini ya kichwa cha habari kisemacho, “Taarifa ya Siri ya
Chadema” ni ya chama hicho au la.
Zitto aliyekuwa akizungumzia matokeo ya ziara yake ya kufuatilia
fedha zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki za Uswisi na
kwingineko Ulaya, alieleza kusikitishwa na kile alichodai kuwa ni
kikundi cha watu ndani ya Chadema ambacho kimekuwa mstari wa mbele
kumpaka matope.
“Wakati nafanya kazi hii ya hatari ya kufuatilia hizo fedha
zilizofichwa nje ya nchi, navunjwa nguvu na watu ambao tuko chama kimoja
kwani imekuwa ni kawaida unapofanya siasa, lazima upate mashambulio na
sasa nashambuliwa na chama changu.
“Katika hali ya kawaida, wenzagu tulionao katika chama ndiyo
waliopaswa kunipa nguvu kwa vile tuna kazi kubwa ya kupambana na ‘lidude
likubwa linaloitwa CCM,” alisema Zitto.
Bila kutaja jina la mtu, alisema kuna watu wachache ambao hawana kazi
ndani ya chama hicho ambao shughuli yao imekuwa ni kugonganisha
viongozi wagombane.
Akirejea historia ya kuchafuliwa kwake, Zitto alisema hali hiyo
ilianza mwaka 2009 baada ya kujitokeza kutaka kugombea uenyekiti wa
Chadema akichuana na Freeman Mbowe.
Chanzo: Mtanzania
Alisema alikuwa ameshamwandikia barua Katibu Mkuu wake, Dk. Willbrod
Slaa akihoji iwapo taarifa ya kumchafua iliyosambazwa katika mitandao ya
intaneti chini ya kichwa cha habari kisemacho, “Taarifa ya Siri ya
Chadema” ni ya chama hicho au la.
Zitto aliyekuwa akizungumzia matokeo ya ziara yake ya kufuatilia
fedha zilizofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki za Uswisi na
kwingineko Ulaya, alieleza kusikitishwa na kile alichodai kuwa ni
kikundi cha watu ndani ya Chadema ambacho kimekuwa mstari wa mbele
kumpaka matope.
“Wakati nafanya kazi hii ya hatari ya kufuatilia hizo fedha
zilizofichwa nje ya nchi, navunjwa nguvu na watu ambao tuko chama kimoja
kwani imekuwa ni kawaida unapofanya siasa, lazima upate mashambulio na
sasa nashambuliwa na chama changu.
“Katika hali ya kawaida, wenzagu tulionao katika chama ndiyo
waliopaswa kunipa nguvu kwa vile tuna kazi kubwa ya kupambana na ‘lidude
likubwa linaloitwa CCM,” alisema Zitto.
Bila kutaja jina la mtu, alisema kuna watu wachache ambao hawana kazi
ndani ya chama hicho ambao shughuli yao imekuwa ni kugonganisha
viongozi wagombane.
Akirejea historia ya kuchafuliwa kwake, Zitto alisema hali hiyo
ilianza mwaka 2009 baada ya kujitokeza kutaka kugombea uenyekiti wa
Chadema akichuana na Freeman Mbowe
Saturday, 16 November 2013
ZITO APEWA ULINZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment