Ni
jambo lisilofichika kwamba watu wengi hujaribu kufanya diet pasipo
mafanikio.Wengi huanza kwa nguvu nyingi na malengo makubwa lakini juhudi
hizo hazifiki mbali.
Ukweli nikwamba kufanya diet ni ngumu,na kuna mambo mengi yanayochangia ugumu huo:
kutokujua aina ya vyakula vinavyofaa
– Wengi hushindwa kufanya diet kwa muda mrefu kwani hajui chakula gani
humfaa zaidi,matokeo yake wengi hushinda njaa au laa hula matunda na
mboga tu na mwisho wasiku njaa huwa kali,mwili hudhoofika na wanaacha
diet.
Gharama ya vyakula hivyo – Diet nyingi huwa na ratiba ya kula pamoja na aina ya vyakula unavyotakiwa kula kwa kila mlo.Mara nyingi vyakula hivi huwa na gharama kubwa au laa huongeza gharama katika familia na kufanya wengi washindwe diet hizo.
Njaa kali – Diet nyingi huelekeza mtu ale chakula kidogo sana,na wakati mwingine vyakula hivi havishiki tumbo kwa muda mrefu au laa mtu hapati kushiba.hivyo huwa na njaa kali muda wote.hali hii uchosha na huwa kama mateso,wengi huacha diet kwa kushindwa kuvumilia hali hii.
Hamu ya kula vyakula wanavyokula wengine hapo nyumbani – Harufu nzuri na muonekanoo wa chakula wanachokula wengine hapo nyumbani mara nyingi huleta hamu ya kula na pia huongeza njaa,hii ufanya wengi waharibu diet zao kwa kula vyakula hivyo ambavyo si sehem ya diet zao.
Ugumu wa kuacha vyakula unavyovipenda – Ni wazi kabisa kwamba ni ngumu sana kuacha kula vyakula unavyovipenda na ulivyovizoea.Ni ngumu zaidi kama kuna aina fulani ya chakula ambayo imekua kama kilevi kwako.Mfano kuna watu asipokunywa soda fulani au juice fulani basi siku kwake haijaisha.
Kuvunjwa moyo na wanaokuzunguka – Mara nyingi watu wanaokuzunguka hukuvunja moyo kwa maneno yao,hasa pale unapofanya juhudi alafu wanakwambia hakuna mabadiliko au laa wengine hudiriki hata kukwambia wewe huwezi kupungua.
Kutaka matokeo ya haraka – wengi wanataka kupunguza mzito mkubwa kwa muda mfupi jambo ambalo si rahisi,Ingawa juhudi zako huchangia uaraka wa kupungua
Uzito mkubwa – uzito mkubwa sana unafanya Mtu aone haiwezekani kupungua kwani inachukua muda mrefu kuona matokeo makubwa.Ni vyema kujua kua kila hatua ndogo unayochukua husaidia,na matokea huja baada ya muda.
Kero – mara nyingi marafiki na ndugu huwa kero kwa maneno yao hasa pale wanapotaka kukwambia fanya nini na uache nini ili upungue.Ni vyema kujua kwamba unapoona ndugu au rafiki ameamua kupunguza uzito basi anasababu za kufanya hivyoo na anajua ni nini afanye au asifanye ili apungue.Naamini kwamba pale anapoitaji msaada wako basi ataomba msaada.Wazungu husema STAY OUT OF OTHER PEOPLES BUSINESS
Ni haya na mengine mengi yanayochangia wengi kushindwa kufanya Diet.Mimi ni mmoja wa wale waliokumbana na hayo yote na kwa njia moja au nyingine yalinirudisha nyuma sana na kunikera.
Baada ya muda mrefu wa kutafuta namna ya kufanya diet endelevu ,kusoma vitabu vingi na kufuata program nyingi za kupunguza uzito atimae nilipata diet ambayo inaweza kukabiliana na changamoto hizo zote nilizozitaja.
Imechapishwa na NewLife Afya
0 comments:
Post a Comment